HABARI MPYA LA JANA MATANGAZO BEI ZETU WASILIANA NASI TUMA HABARI
ijumaa, 14 septemba 2012
Yaliyopita
Pekua Tovuti

Cool Boy ajivunia video ya Jigijigi


na Mwandishi wetu

 

MKALI wa kibao cha ‘Mtoto wa Geti Kali’, Amiry Ally Baruti ‘Cool Boy’, amekamilika video ya wimbo wake wa ‘Jigijigi’ na kutamba kuwa kibao hicho kitamtambulisha tena katika anga ya muziki wa kizazi kipya.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Cool Boy alisema, ana kila sababu ya kujivunia video hiyo, kwani imerekodiwa katika viwango vya hali ya juu na kila aliyefanikiwa kuiona, hakusita kuisifia.

Cool Boy alisema, sababu za kujivunia video hiyo ni kutokana na kuirekodi katika mandhari nzuri na zenye mvuto wa kuendelea kuiangalia mara kwa mara.

“Nina kila sababu za kujivunia video ya wimbo wangu wa Jigijigi, kwani ni nzuri na inashawishi kuendelea kuiangalia kila wakati na hii ni salamu kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya,” alisema.

Msanii huyo aliongeza kuwa, anaamini ubora wa video hiyo utaleta ushindani mkali katika muziki wa kizazi kipya na hilo limeanza kujidhihirisha baada ya kuanza kupokea mialiko ya kwenda kufanya shoo maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.



juu