logo spc.r_ad0
sp.b_ad0
blu.strip
spc.bt_blu.strip
HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
sp.b_menu
ban
sp.b_ban
jumatatu, 11 septemba 2006
Pekua Tovuti
sp.t_sech.box sp.tafuta_w_tuma sp.t_tuma sp.r_tuma
sp.b_box sp.b_tuma
sp.b_F1
h.sep1
sp.r_men
sp.t
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari
sp.b_tuma
sp.l_men
h.sep1
sp.l sp.t sp.r
LOGIN
sp.men.l sp.men.t sp.men.r
Username
sp.b_user
sp.t-word
Password
sp.b_word
sp.t_btn
sp.b_btn
sp.b
h.sep1
tp.spc

Wana apolo walaani migodi kufungwa


Na David Frank, Arusha

WACHIMBAJI wadogo wa madini ya tanzanite, maarufu kama Wana-apolo, Mererani wilayani Simanjiro, Manyara, wamelaani kitendo cha Wizara ya Nishati na Madini kuwahukumu kwa kuwafungia migodi yao hata kabla uchunguzi wa madai ya ulipukaji wa mabomu katika migodi hiyo haujakamilika.

Wakati wachimbaji wadogo wakifungiwa uchimbaji, wenzao wa Kampuni ya TanzaniteOne wanaendelea kuchimba.

Kufungiwa kwa migodi hiyo ya wachimbaji wadogo, kumeelezwa ni hatari kwani zaidi ya Wana-apolo 1,000 hawana kazi za kufanya, hali iliyodaiwa inaweza kusababisha vurugu na upotevu wa amani baada ya kukosa masurufu ya kujikimu kimaisha.

“Migodi ya wachimbaji wadogo imefungwa, sawa, lakini kwanini ifungwe hiyo tu, wakati madai ya ulipukaji wa bomu yalitokea katika migodi ya wachimbaji wakubwa na hakuna hata mitobozano inayoonyesha kuwa wachimbaji wadogo walipenya na kwenda kulipua mabomu hayo?” alihojia mmoja wa Wana-apolo ambaye hakutaka kutajwa jina.

Baadhi ya wataalamu wa machimbo hayo wamedai hali hiyo inaweza kusababisha tafrani na kwamba zipo taarifa zisizothibitishwa zinazodai Wana-apolo hao wanaweza kuvamia sehemu za biashara ndogo ndogo katika machimbo, kwani tayari kina mama lishe wameanza kulia baada ya kudhulumiwa vyakula na wachimbaji hao.

Migodi 17 ya wachimbaji wadogo ilifungiwa wiki iliyopita kwa kile kilichoelezwa hadi uchunguzi ufanyike jambo linalopigiwa kelele na wachimbaji hao.

 


h.sep

juu sp.b
Habari Mpya  |  Kitaifa  |  Dar  |  Mikoani  |  Tahariri  |  Makala  |  Michezo  |  Matangazo  |  Webmaster
Copyright 2006 © FreeMedia Ltd.
Free media limited
mtaa wa mkwepu na makunganya, slp 15261, dar es salaam, tanzania
simu +255-22-2120604  •  faksi +255-22-2126234