logo spc.r_ad0
sp.b_ad0
blu.strip
spc.bt_blu.strip
HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
sp.b_menu
ban
sp.b_ban
jumanne, 12 septemba 2006
Pekua Tovuti
sp.t_sech.box sp.tafuta_w_tuma sp.t_tuma sp.r_tuma
sp.b_box sp.b_tuma
sp.b_F1
h.sep1
sp.r_men
sp.t
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari
sp.b_tuma
sp.l_men
h.sep1
sp.l sp.t sp.r
LOGIN
sp.men.l sp.men.t sp.men.r
Username
sp.b_user
sp.t-word
Password
sp.b_word
sp.t_btn
sp.b_btn
sp.b
h.sep1
tp.spc

Iran yafikiria kusitisha nyuklia


VIENNA, Austria

WANADIPLOMASIA wanaoshughulikia mzozo wa nyuklia wa Iran, wamefichua kwamba Serikali ya Iran iko tayari kufikiria usitishaji wa shughuli za kurutubisha madini ya uranium kwa kipindi cha miezi miwili.

Wanadiplomasia hao waliosisitiza kutotajwa majina kutokana na unyeti wa suala hilo, walisema hayo muda mfupi baada ya wanadiplomasia waandamizi wa Iran na Jumuiya ya Ulaya (EU) kufanya mazungumzo ya pili juu ya upuuzaji uliofanywa na Iran kutii azimio la UN linaloitaka nchi hiyo kusitisha urutubishaji wa madini ya uranium yanayoweza kutumika katika utengenezaji wa mabomu ya nyuklia.

Alisema kwamba kauli hiyo ilitolewa na mpatanishi mkuu wa nyuklia wa Iran, Ali Larijani, wakati alipokutana na mkuu wa sera za nje wa EU, Javier Solana.

Mwanadiplomasia mmoja alisema kwamba Larijani aligusia uwezekano wa kusitisha shughuli za urutubishaji wa uranium, kwa mwezi au miezi miwili iwapo haitashinikizwa.

Iwapo hilo litafikiwa itakuwa hatua nzuri kufikiwa katika mazungumzo hayo na Iran, ambayo iko katika tishio la kuadhibiwa kwa kupuuza azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kusitisha programu hiyo iliyokuwa imewekewa tarehe ya mwisho Agosti 31.

Mapema, Larijani na Solana walizungumzia maendeleo ya majadiliano yao na walikubaliana kukutana tena baadaye wiki hii.

Mazungumzo yao yalikuwa yakipewa nafasi finyu ya kufanikiwa baada ya miezi kadhaa ya kuongezeka kwa mgogoro juu ya suala hilo.

Lakini pande zote mbili hazikugusia hadharani kile walichokubaliana katika mazungumzo hayo zaidi ya Solana kusema kwamba majadiliano yao yalitia moyo huku Larijani akisema hali ya shaka juu ya Iran imeondolewa.

“Tumefikia mahali pazuri katika masuala kadhaa,” Larijani alisema.

Mkutano huo unaonekana kuipatia Iran fursa ya kuepuka adhabu ya UN baada ya mazungumzo hayo kuonekana kuzaa matunda pamoja na kwamba hayajawekwa hadharani.

Iran imekuwa ikisisitiza kwamba programu yake ya nyuklia ni kwa ajili ya amani wakati nchi za magharibi zinasema kuwa inalenga kutengeneza silaha za nyuklia.

CNN

 


h.sep

juu sp.b
Habari Mpya  |  Kitaifa  |  Dar  |  Mikoani  |  Tahariri  |  Makala  |  Michezo  |  Matangazo  |  Webmaster
Copyright 2006 © FreeMedia Ltd.
Free media limited
mtaa wa mkwepu na makunganya, slp 15261, dar es salaam, tanzania
simu +255-22-2120604  •  faksi +255-22-2126234