logo spc.r_ad0
sp.b_ad0
blu.strip
spc.bt_blu.strip
HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
sp.b_menu
ban
sp.b_ban
jumanne, 12 septemba 2006
Pekua Tovuti
sp.t_sech.box sp.tafuta_w_tuma sp.t_tuma sp.r_tuma
sp.b_box sp.b_tuma
sp.b_F1
h.sep1
sp.r_men
sp.t
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari
sp.b_tuma
sp.l_men
h.sep1
sp.l sp.t sp.r
LOGIN
sp.men.l sp.men.t sp.men.r
Username
sp.b_user
sp.t-word
Password
sp.b_word
sp.t_btn
sp.b_btn
sp.b
h.sep1
Tanzania haiwezi kujengwa na wageni
Happiness Katabazi


UPO msemo unaosema kwamba ‘mjenga nchi ni mwananchi na mbomoa nchi ni mwananchi’.

Usemi huu haufichui ukweli kwamba hakuna nchi iliyowahi kujengwa na wageni, lakini zipo nchi zilizowahi kubomolewa na wageni.

Kwa hiyo, kila mara taifa lolote hutoa kipaumbele katika kujilinda dhidi ya vitendo vya hujuma vinavyoweza kufanywa na wageni.

Katika sayansi ya ulinzi, majeshi ya ulinzi huwa yenye nguvu kubwa kuliko Jeshi la Polisi na Magereza.

Hivi sasa sayansi ya ulinzi imefikia viwango vya kuruhusu majeshi ya ulinzi kuwa sehemu ya jeshi la kujenga na kulinda taifa.

Hivyo, majeshi ya ulinzi hayatumiki tu vitani bali wakati wa amani majeshi hayo hutumika kujenga taifa. Na majeshi yetu ya ulinzi ni Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Majeshi yetu hayo kwa karne hii nakiri kuwa yana wasomi na wataalamu wengi, ambao kama wangeyatumikia vizuri, yangeliletea taifa maendeleo makubwa.

Kwa mfano, majeshi haya yana vikosi vya ukandarasi ambavyo vina uwezo mkubwa wa kujenga barabara, madaraja, mabwawa ya maji, majosho ya kuoshea mifugo, mifereji, majengo na mengine.

Vikosi hivi vya ukandarasi hutumika kwa kazi za kiraia wakati wa majanga tu, na aieleweki ni kwanini nguvu kazi hii bora na adimu haitumiwi na serikali kuleta maendeleo wakati mwingine, si lazima wakati wa majanga.

Wasiwasi ni kuwa wakiyahusisha haya majeshi, hawa wakubwa watakosa tenda na bahasha zao.

Hayo ndiyo matokeo ya ufisadi ndani ya serikali yetu, tupo tayari kutoa tenda ya ujenzi wa barabara kwa wageni, hata kama wageni hao wanatumia wafungwa kutoka nchini mwao kuliko kutumia kile kilicho chetu. Kwa hakika tunajiuza kwa bei rahisi mno mithili ya nazi sokoni.

Katika majeshi yetu, tuna Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), ambalo hadi sasa halitumiwi vizuri. Tulitarajia kuona wanajeshi wa majeshi yetu wanapewa mafunzo ya kitaalamu na ufundi na kisha wasambazwe nchi nzima kushirikiana na wananchi kujenga shule, zahanati, vyuo, hospitali, masoko, barabara na mambo mengine.

Tulitarajia pia kuona wanajeshi hawa wenye ujuzi na stadi za maisha, wakisambazwa nchi nzima kutoa mafunzo kwa vijana wetu ili waweze kuanzisha shughuli zao za kujitegemea kiuchumi, lakini hayo hayafanyiki na jeshi tunalo.

Tunalo Jeshi la Magereza, lenye wafungwa wanaofurika kila kukicha. Tulitarajia kuona jeshi hilo likitumika kama chuo cha mafunzo kuwafunza wafungwa hao shughuli za kiuchumi na kuwaandaa kuwa raia wema mara wamalizapo kipindi chao cha kifungo.

Tunachokiona ni wafungwa wasio na ujuzi wanaomaliza kutumikia kifungo chao na kurudi uraiani na kurejea tena kufanya vitendo vya uhalifu ule ule, tena kwa kasi ya ajabu.

Kwa kuwa Rais Jakaya Kikwete ni Amiri Jeshi Mkuu na alishawai kuwa mwanajeshi, hivyo kaulimbiu yake ya Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya, ianzie huko jeshini. Tunataka tuwaone wanajeshi wetu wakichacharika kama wanajeshi wa Korea na Cuba, ambao wamezisaidia nchi zao kupata maendeleo makubwa.

Kwa mtazamo wangu, kuendelea kuwaacha wanajeshi wetu hivi walivyo, ni hasara kubwa kwa taifa, kwani jukumu lao si kupigana vita tu bali tunapaswa pia kutumia taaluma na nguvu zao wakati huu wa amani.

Tunajua kuna hoja kwamba majeshi yetu hayana vifaa vya kuweza kutekeleza tenda mbalimbali za ukandarasi, mbona hao makandarasi wanaopewa tenda za ujenzi, hununua vifaa kutokana na fedha hiyo pindi wanapopata tenda?

Sasa kuna faida gani fedha ya mlipa kodi wa Tanzania itumike kumwezesha mkandarasi wa nje kununua vifaa badala ya kumruhusu Mtanzania kutumia fedha hiyo hiyo kununulia vifaa?

Ieleweke kuwa tenda hizi zikitolewa kwa mkandarasi wa Kitanzania, zitakuwa ni nafuu, tena zitaendelea kuwa nafuu kadiri watakavyoendelea kupata vifaa vya kisasa.

Aidha, tenda hizi zikitolewa kwa majeshi yetu zitakuwa rahisi, kwa kuwa wao wana nguvu kazi na mfumo wa ukakamavu na nidhamu ya hali ya juu katika utendaji na utekelezaji wa kazi waliyopewa kuifanya.

0755-312859
Email;
katabazihappy@yahoo.com

h.sep
juu sp.b
Habari Mpya  |  Kitaifa  |  Dar  |  Mikoani  |  Tahariri  |  Makala  |  Michezo  |  Matangazo  |  Webmaster
Copyright 2006 © FreeMedia Ltd.
Free media limited
mtaa wa mkwepu na makunganya, slp 15261, dar es salaam, tanzania
simu +255-22-2120604  •  faksi +255-22-2126234