logo spc.r_ad0
sp.b_ad0
blu.strip
spc.bt_blu.strip
HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
sp.b_menu
ban
sp.b_ban
jumapili, 11 Novemba 2007
Pekua Tovuti
sp.t_sech.box sp.tafuta_w_tuma sp.t_tuma sp.r_tuma
sp.b_box sp.b_tuma
sp.b_F1
h.sep1
sp.r_men
sp.t
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari
sp.b_tuma
sp.l_men
h.sep1
sp.l sp.t sp.r
LOGIN
sp.men.l sp.men.t sp.men.r
Username
sp.b_user
sp.t-word
Password
sp.b_word
sp.t_btn
sp.b_btn
sp.b
h.sep1
tp.spc


Serikali yamtosa Rubeya na wenzake


na Eugeni Kimolo


SERIKALI kupitia Kamati ya Michezo Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, imebatilisha maamuzi ya wanachama wa klabu ya Simba, ya kuusimamisha uongozi ulio chini ya Mwenyekiti Hassan Dalali, Novemba 4.

Uamuzi huo umefikiwa juzi jioni na kamati hiyo iliyokuwa imekutana kujadili suala hilo baada ya uongozi wa Dalali kuwasilisha malalamiko kwa Msajili Msaidizi wa Vyama na Klabu na Michezo Wilaya ya Ilala, ukipinga kusimamishwa huko.

Katibu Mwenezi wa klabu hiyo, Said Rubeya ‘Seydou’, aliyeitisha mkutano huo wa Jumapili, aliwasilisha taarifa kwa msajili huyo akijenga hoja kuwa maamuzi yaliyofanywa na wanachama ni halali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa Kamati hiyo ya Michezo, Penina Maduhu aliye pia Msajili Msaidizi wa Vyama na Klabu za Michezo Wilaya ya Ilala, mkutano wa Jumapili ni batili kwa mujibu wa katiba.

Maduhu alisema, baada ya kupitia Katiba ya Simba ya mwaka 1988, kamati hiyo ilibaini mapungufu mengi ambayo kwayo, mkutano wa Jumapili ni batili kwa mujibu wa Ibara ya 7.7.1 ya katiba hiyo.

Ibara hiyo inasema: “Mikutano ya jumla ya wanachama itatambuliwa na vikao vya juu na vya mwisho vya klabu ambavyo ni mikutano wa dharura, itakayoitishwa na Kamati ya Utendaji kama kuna haja ya kufanya hivyo.

“Mikutano ya kila baada ya miezi minne na mkutano mkuu wa mwaka. Kwa maana hiyo, mkutano ulioitishwa kama ukiitwa wa dharura kwa mujibu wa kifungu cha ibara hii, unahitaji ridhaa ya kamati ya utendaji.”

Taarifa hiyo ilisema kama mkutano wa Jumapili iliyopita ulikuwa wa kawaida ambao huitishwa kila baada ya miezi minne kwa mujibu wa kifungu 6.2 (iii), ulipaswa kuitishwa na Katibu Mkuu, isipokuwa kamati ndogondogo.

Aidha, kwa mujibu wa kipengele 6.5, manaibu Mwenyekiti, Katibu Mkuu na Mweka Hazina hufanya shughuli zote zinazohusika na wakuu hao kama tu wahusika wamesafiri, wagonjwa au hawajiwezi kwa njia yoyote ile.

“Kwa kipengele hiki, kwa kutokuwepo Katibu Mkuu ambaye angeweza kuitisha mkutano, mkutano husika ulipaswa kuitishwa na Katibu Msaidizi na si kiongozi mwingine yeyote kwa mujibu wa katiba, hivyo mkutano wa Jumapili iliyopita hauna sifa ya kuitwa mkutano wa kawaida.

“Pia, baada ya kupitia kumbukumbu za Simba, tumeona wameshaitisha mikutano miwili ya kawaida na kwa vile mwaka haujaisha, hatutarajii mkutano huo ulikuwa mkutano mkuu wa mwaka ambao pia huitishwa na Katibu Mkuu.”

Taarifa hiyo ilisema, kikao cha mkutano wa mwisho wa wanachama ulikuwa ni Agosti 26, 2007, hivyo kwa mujibu wa katiba kwa vile vikao viwili vimeshafanyika, usimamishwaji wa Dalali na wenzake watano ni batili kikatiba.

Kwa vile mkutano uliofanyika ni batili, hivyo hata maamuzi ya kumsimamisha Dalali na wenzake, ni batili na uongozi unaotambuliwa ni ule ulioingia madarakani Desemba 3, mwaka 2006.

Uamuzi wa serikali umekuja huku kinara wa mapinduzi hayo, Rubeya akiwa ametangaza Kamati ya Muda ya wajumbe 17, ingawa wengine walikataa uteuzi huo kwa hoja kuwa kung’olewa kwa Dalali, ni batili.


h.sep

juu sp.b
Habari Mpya  |  Kitaifa  |  Dar  |  Mikoani  |  Tahariri  |  Makala  |  Michezo  |  Matangazo  |  Webmaster
Copyright 2007 © FreeMedia Ltd.
Free media limited
mtaa wa Mkwepu na Makunganya, jengo la Bilicanas, gorofa ya kwanza, SLP 15261, Dar es salaam, Tanzania
simu +255-22-2126233  •  faksi +255-22-2126234  •  Selula  0713 296570