logo spc.r_ad0
sp.b_ad0
blu.strip
spc.bt_blu.strip
HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
sp.b_menu
ban
sp.b_ban
jumamosi, 15 Desemba 2007
Pekua Tovuti
sp.t_sech.box sp.tafuta_w_tuma sp.t_tuma sp.r_tuma
sp.b_box sp.b_tuma
sp.b_F1
h.sep1
sp.r_men
sp.t
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari
sp.b_tuma
sp.l_men
h.sep1
sp.l sp.t sp.r
LOGIN
sp.men.l sp.men.t sp.men.r
Username
sp.b_user
sp.t-word
Password
sp.b_word
sp.t_btn
sp.b_btn
sp.b
h.sep1
tp.spc


Mwekezaji mpya RTL lawamani Tanga


na Anna Makange, Tanga


SERIKALI imeombwa kuchukua hatua za haraka za kulinusuru Shirika la Reli Mkoa wa Tanga ambako ofisi yake imefungwa na watumishi wote kuondolewa kazini kwa zaidi ya miezi miwili baada ya shirika hilo kubinafsishwa.

Ombi hilo lilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mohamed Abdulaziz, wakati wa mazungumzo ya pamoja kati ya madiwani, watendaji wakuu wa halmashauri ya mji huo na Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

Mkuu huyo, alimtahadharisha Waziri Mkuu kuwa iwapo jitihada za haraka hazitafanyika, baada ya muda mfupi upo uwezekano wa baadhi ya vyuma vya reli za mkoa huu kufunguliwa na wahalifu kisha kuuzwa kama chuma chakavu.

Alisema, jambo hilo litachangia kwa kiasi kikubwa kurudisha nyuma maendeleo ya mkoa na serikali kupata hasara na akamweleza Waziri Mkuu kwamba, tegemeo la watumishi wa reli ni kuboreshewa miundombinu na hali za maisha yao baada ya kuingia mwekezaji jambo ambalo ni kinyume na matarajio.

“Waziri Mkuu, tegemeo langu lilikuwa kwamba baada ya shirika hilo kubinafsishwa mwekezaji, basi angelenga katika kuboresha huduma mbalimbali za miundombinu ya kiutendaji.

“…Pia tulitegemea ongezeko la safari za treni za mizigo kutoka bandarini, badala yake ameamua kufunga ofisi na kuwaondoa watumishi wote mpaka walinzi, inasikitisha. Jambo hili litaathiri mapato yetu na kuporomosha uchumi wa Mkoa wa Tanga,” alifafanua Abdulaziz.

Alibainisha kuwa, ofisi yake imeiandikia Wizara ya Miundombinu barua kuhusu tatizo hilo na kuliwasilisha kikaoni hapo ili Lowassa, aliunge mkono na kutafuta njia mbadala ya kulinusuru shirika hilo.

Mkuu huyo alisema, azma ya serikali kuu ni kuona serikali za mitaa zinajiendeleza kwa lengo la kuwarahisishia wananchi upatikanaji wa huduma bora.

“Wanafahamu kwamba serikali imedhamiria kuboresha maisha yao na hali ya usafirishaji wa njia ya reli kwa kujenga bandari ya Tanga, katika eneo la Mwambani na ujenzi wa barabara ya Tanga-Horohoro… lakini naomba niseme kwamba haya yote yatafanikiwa iwapo tu na reli yetu itafanya kazi,” alisisitiza.


h.sep

juu sp.b
Habari Mpya  |  Kitaifa  |  Dar  |  Mikoani  |  Tahariri  |  Makala  |  Michezo  |  Matangazo  |  Webmaster
Copyright 2007 © FreeMedia Ltd.
Free media limited
mtaa wa Mkwepu na Makunganya, jengo la Bilicanas, gorofa ya kwanza, SLP 15261, Dar es salaam, Tanzania
simu +255-22-2126233  •  faksi +255-22-2126234  •  Selula  0713 296570