KAMBI ya Upinzani bungeni jana iliwasilisha bajeti mbadala ikijibu hoja za Waziri wa Fedha, Zakia Meghji na Waziri wa Mipango, Uchumi na Uwezeshaji, Dk. Juma Ngasongwa. Waziri Kivuli wa Fedha, Hamad Rashidi Mohamed (Wawi-CUF), alieleza kusikitishwa kwake na matumizi makubwa na yasiyo na tija serikalini...
TULIANDIKA, tukaandika tena na sasa tunaandika kwa mara nyingine, tukijua vyema kwamba Bunge la Bajeti linakutana Dodoma. Kama tulivyopata kuahidi siku zilizopita, tunaamini kwamba, Rais Kikwete, mawaziri wake na wabunge kwa ujumla wao walisikia kile tunachokililia na kimsingi tutaendelea kulipigania hilo hadi hapo tutakapoona limemalizika na kuhitimishwa...
KATIKA makala yangu ya mwisho ya mfululizo huu kuhusu Katiba, nilimalizia kwa kuahidi kwamba makala ifuatayo ningeandika kuhusu Tume ya Uchaguzi. Kutokana na tuhuma au kudhihirika hivi karibuni kwamba haki, fadhila na madaraka ya rais yametumiwa vibaya kujinufaisha binafsi...
SERIKALI imebainisha kuwa jumla ya sh bilioni 1.6 zilitumika katika semina elekezi kwa viongozi wa serikali katika Hoteli ya Ngurdoto mkoani Arusha mwaka jana...
AGIZO la Waziri Mkuu, Edward Lowassa, juu ya ukarabati wa taa za barabarani, limekwama kwa kile kilichoelezwa kuwa ni wimbi la wizi wa vifaa vya taa hizo...
KAMA ilivyotarajiwa, wabunge wengi walioanza kuchangia bajeti ya 2007/08 jana jioni, wameonyesha kutoridhishwa kwao na ongezeko la ushuru katika bidhaa za mafuta ya aina zote...
WAANDISHI wa habari, Mariam Nkya, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo cha Uandishi wa Habari, Dar es Salaam School of Journalism (DSJ), na Safina Kassanga wa Kampuni ya Mwananchi Communications, juzi usiku waling’ara katika kinyang’anyiro cha Miss Ukonga 2007....
HAKIKA, haijapata kutokea, wachezaji wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, jana walichangiwa jumla ya sh mil. 322.5 katika harambee iliyosimamiwa na Waziri Mkuu, Edward Lowassa, mjini Dodoma...