logo spc.r_ad0
sp.b_ad0
blu.strip
spc.bt_blu.strip
HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
sp.b_menu
ban
sp.b_ban
jumatano, 20 Juni 2007
Pekua Tovuti
sp.t_sech.box sp.tafuta_w_tuma sp.t_tuma sp.r_tuma
sp.b_box sp.b_tuma
sp.b_F1
h.sep1
sp.r_men
sp.t
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari
sp.b_tuma
sp.l_men
h.sep1
sp.l sp.t sp.r
LOGIN
sp.men.l sp.men.t sp.men.r
Username
sp.b_user
sp.t-word
Password
sp.b_word
sp.t_btn
sp.b_btn
sp.b
h.sep1


Katika hili tunakubaliana na wabunge wa upinzani



JUZI wabunge wa kambi ya upinzani waliwasilisha kile walichokielezea kuwa ni bajeti mbadala iliyokuwa ikijibu hotuba ya bajeti ya Waziri wa Fedha, Zakia Meghji aliyoitoa Alhamisi ya wiki iliyopita.

Wabunge hao wa upinzani katika mapendekezo yao hayo waliitaka serikali kuitengea sekta ya miundombinu kiwango kikubwa zaidi cha fedha kinachozidi asilimia 20 ya bajeti nzima.

Mapendekezo hayo ya wabunge yanakinzana na yale ya serikali ambayo yaliiweka sekta hiyo kuwa ni ya tatu baada ya elimu na afya ikitengewa asilimia 10 tu.

Kwa maelezo yao wapinzani katika mapendekezo yao hayo, ambayo kimsingi tunayaunga mkono, walisema miundombinu ni sekta muhimu itakayoweza kufanikisha azima ya serikali kukabiliana na umaskini hapa nchini.

Kwa wapinzani, miundombinu ni sekta ambayo kwa kiwango kikubwa inaweza kutoa nafasi kubwa ya kuendeleza kilimo ambacho kwa miaka zaidi ya 45 ya uhuru wetu tumekuwa tukikisema midomoni tu kuwa ndiyo uti wa mgongo.

Wakati tukiwapongeza wabunge wa upinzani kwa mtazamo wao huo, tunapenda kuikumbusha Serikali ya Awamu ya Nne kukumbuka na kuendeleza mema ambayo yalifanywa na serikali iliyotangulia.

Tunasema hivyo kwa sababu miezi michache tu iliyopita, katika safu hii ya tahariri tulipata kuiuliza serikali ya Kikwete kuhusu kupungua kwa kasi ya ujenzi wa barabara ambayo ilikuwa ikionekana zama za Rais mstaafu Benjamin Mkapa.

Ingawa ni kweli kwamba, mipango kadhaa ya Serikali ya Awamu ya Tatu kukamilisha ujenzi wa barabara mbalimbali muhimu haukwenda kama ilivyokuwa ikielezwa, bado kulikuwa na mafanikio kadha wa kadha yaliyokuwa yakijionyesha kwa uwazi kabisa kuwa kazi ilikuwa ikifanyika.

Moja ya ndoto za wazi ambazo zilikuwa zikipigiwa chapuo na Mkapa mwenyewe na aliyekuwa waziri wake wa Ujenzi, John Magufuli, na ambayo imekwama, ilikuwa ni ile ya kuona magari madogo aina ya saloon yakiwa na uwezo wa kusafiri kwa njia ya barabara ya lami kuanzia Mtwara hadi Mwanza kipindi hiki.

Si hilo tu, jingine lilikuwa ni lile la serikali hiyo ya Mkapa kufikia mahali ikatamba kwamba, ilikuwa imefikia hatua ya kutenga fedha zinazotokana na mapato ya ndani katika ujenzi wa barabara hizo pasipo kusubiri misaada au hisani ya wafadhili.

Kwa maelezo yoyote yale, ujenzi wa barabara ulikuwa ukionekana kuwa eneo lililokuwa na mafanikio makubwa pengine kuliko maeneo mengine yote ya kiutendaji serikalini.

Dhamira ya serikali ya CCM kuweka mkazo katika ujenzi wa barabara ilishaanza kuonyeshwa mapema kabisa na Serikali ya Awamu ya Pili ya mzee Ali Hassan Mwinyi hata kabla Mkapa hajaingia madarakani.

Baadhi yetu tungali tukikumbuka vyema namna ilivyokuwa mwaka 1996 wakati Mkapa alipokuwa akikabidhiwa madaraka ya kukiongoza chama hicho kutoka kwa mzee Mwinyi pale alipoahidi kuwa ataendeleza dhamira ya kuupa ujenzi wa barabara kipaumbele cha kwanza, pili na cha tatu kama alivyowahi kuahidi mtangulizi wake wakati alipotembelea nchini Ujerumani wakati yeye akiwa Waziri wa Mambo ya Nje.

Kwa sababu ya ukweli huo, ni matarajio ya kawaida kwamba, moja ya mambo ambayo tungeona yakifanywa kwa kasi ile ile ya CCM ya Mwinyi, Mkapa na Magufuli ingeendelezwa wakati huu wa Serikali ya Awamu ya Nne ya CCM ya kina Kikwete na Andrew Chenge.

Kwa bahati mbaya hali inaonekana kuwa ni tofauti, kwani kwa kipindi chote wananchi hawajaonyeshwa kwa uwazi kuendelezwa kwa kasi ile ya zama za Mwinyi na baadaye Mkapa.

Ni kwa sababu hiyo ndiyo maana tunakubaliana kwa asilimia 100 na mtazamo wa wabunge wa upinzani wa kuikumbusha serikali hii ya sasa kutoisahau sekta nyeti ya miundombinu ambayo uimarishwaji wake utakuza uchumi wetu.


h.sep
juu sp.b
Habari Mpya  |  Kitaifa  |  Dar  |  Mikoani  |  Tahariri  |  Makala  |  Michezo  |  Matangazo  |  Webmaster
Copyright 2007 © FreeMedia Ltd.
Free media limited
mtaa wa Mkwepu na Makunganya, jengo la Billicanas, gorofa ya kwanza, SLP 15261, Dar es salaam, Tanzania
simu +255-22-2126233  •  faksi +255-22-2126234  •  Selula  0713 296570