logo spc.r_ad0
sp.b_ad0
blu.strip
spc.bt_blu.strip
HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
sp.b_menu
ban
sp.b_ban
ijumaa, 10 Agosti 2007
Pekua Tovuti
sp.t_sech.box sp.tafuta_w_tuma sp.t_tuma sp.r_tuma
sp.b_box sp.b_tuma
sp.b_F1
h.sep1
sp.r_men
sp.t
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari
sp.b_tuma
sp.l_men
h.sep1
sp.l sp.t sp.r
LOGIN
sp.men.l sp.men.t sp.men.r
Username
sp.b_user
sp.t-word
Password
sp.b_word
sp.t_btn
sp.b_btn
sp.b
h.sep1
tp.spc


Ubalozi wa Marekani wazindua mtandao


na Tamali Vullu


UBALOZI wa Marekani nchini umezindua mtandao wa masuala ya kielimu (Education Perspectives Chapter) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Sekondari ya Karagwe iliyopo mkoani Kagera.

Balozi wa Marekani nchini, Micahel Retzer, alizindua mtandao huo jana katika ofisi za ubalozi huo, Dar es Salaam baada ya kusaini makubaliano ya kuanzishwa kwa mtandao huo.

Balozi Retzer alisema mtandao huo una lengo la kupanua uelewa wa watu katika masuala mbalimbali.

Alisema ni mara ya kwanza mtandao huo kuzinduliwa barani Afrika na kwamba hivi sasa unafanya kazi katika nchi za China-Hong Kong, Canada na Marekani.

Alisema mtandao huo umeanzishwa katika Chuo Kikuu cha Johns Hopkins na kwamba wanafunzi wa mtandao hao watakuwepo nchini kati ya Agosti 7-24 mwaka huu.

Alisema baadhi ya wanafunzi wa chama hicho wameshakwenda katika Sekondari ya Kagagwe kwa ajili ya kutoa huduma na pia wanatarajiwa kwenda kisiwani Pemba kuzindua mtandao huo katika Sekondari ya Utaani na Chuo cha Benjamin Mkapa kilichopo Wete.

Alisema wanafunzi hao watabadilishana uzoefu wa wanafunzi wa Kitanzaia katika masuala ya afya ukiwemo ugonjwa wa ukimwi, kujifunza tamaduni mbalimbali na masuala ya lugha.

Askofu wa Dayosisi ya Karagwe, Benson Bagonza, alisema chini ya mtandao huo dayosisi yake ambayo inamiliki shule ya sekondari, itaanzisha kliniki za afya kwa ajili ya kuwasaidia watu wasiojiweza.

Alisema kupitia mtandao huo, wanatarajia kuongeza mabweni ya wasichana katika sekondari hiyo kwa lengo la kuwawezesha wasichana wengi zaidi kujiunga.

Aidha, wanatarajia kuazisha Chuo Kikuu cha Kilimo na Mazingira ambacho amesema baada ya miaka mitano ijayo kitakuwa kimekamilika. Alisema wameshapata eneo la ekari 200 kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho na pia wana kibali cha kumiliki eneo hilo.

Akizungumzia mtandao huo, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Colman Msoka, alisema lengo la mtandao huo ni kuwawezesha wanafunzo hao kutoa mchango wao katika jamii.

Alisema ingawa chama hicho katika chuo hicho bado ni kichanga, watajitahidi kushirikiana na waanzilishi wa chama hicho ili kiweze kuendelea.


h.sep

juu sp.b
Habari Mpya  |  Kitaifa  |  Dar  |  Mikoani  |  Tahariri  |  Makala  |  Michezo  |  Matangazo  |  Webmaster
Copyright 2007 © FreeMedia Ltd.
Free media limited
mtaa wa Mkwepu na Makunganya, jengo la Bilicanas, gorofa ya kwanza, SLP 15261, Dar es salaam, Tanzania
simu +255-22-2126233  •  faksi +255-22-2126234  •  Selula  0713 296570