KUNA kila dalili kwamba, mwenendo wa mambo serikalini si mzuri baada ya aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Daudi Ballali, kueleza nia yake ya kutaka kurejea nyumbani kukabiliana na tuhuma zinazomkabili na kuwaweka bayana wahusika wakuu wa sakata hilo...
JUMAPILI iliyopita, tuliandika tukimuomba Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa, avunje ukimya wake, ajitokeze kuzungumzia kashfa kubwa ya upotevu wa mabilioni ya fedha za Watanzania zilizochotwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wakati akiwa kiongozi mkuu wa taifa letu...
JUMANNE, Januari 29, mwaka huu, kikao cha kumi cha Bunge la Jamhuri kinaanza mjini Dodoma chini ya Spika Samuel Sitta. Nimepanga kusafiri kwenda huko nikakutane naye ‘mwishimiwa’ Sitta nizungumze naye machache ...
JESHI la Polisi mkoani Dar es Salaam linawashikilia raia kumi wa Somalia kwa kuishi kinyume cha sheria nchini. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Jamal Rwambow, alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 9:30 katika maeneo mbalimbali ya jiji. ...
DIWANI wa Kata ya Usanda kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Wilaya ya Shinyanga Vijijini, Abeid Ndaji, amesimamishwa uongozi kwa tuhuma za kukiuka kanuni za uongozi baada ya tume iliyoundwa kuchunguza tuhuma hizo kubaini kuwa alitafuna michango ya ujenzi wa shule za sekondari...
HATUA ya serikali ya kuamua kujenga kumbi za kisasa za maonyesho huko Bagamoyo na hapa Dar imepongezwa na kukosolewa na wapenzi wa muziki na sanaa za maonesho. Licha ya kufurahishwa na mpango huo, wadau hao wamehoji mantiki ya uamuzi wa kujenga ukumbi wa kisasa wa maonyesho huko Bagamoyo, mbali na jiji la maraha la Dar es Salaam...
YANGA, jana iliianza vizuri ngwe ya pili ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuifunga Ashanti United mabao 2-1 katika mechi iliyopigwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam...