logo spc.r_ad0
sp.b_ad0
blu.strip
spc.bt_blu.strip
HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
sp.b_menu
ban
sp.b_ban
jumatatu, 28 Januari 2008
Pekua Tovuti
sp.t_sech.box sp.tafuta_w_tuma sp.t_tuma sp.r_tuma
sp.b_box sp.b_tuma
sp.b_F1
h.sep1
sp.r_men
sp.t
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari
sp.b_tuma
sp.l_men
h.sep1
sp.l sp.t sp.r
LOGIN
sp.men.l sp.men.t sp.men.r
Username
sp.b_user
sp.t-word
Password
sp.b_word
sp.t_btn
sp.b_btn
sp.b
h.sep1
tp.spc


TechnoServe kusaidia kilimo cha kahawa


na Mwandishi Wetu


MRADI wa Taasisi ya Maendeleo ya TechnoServe unatarajia kupokea msaada wa dola milioni 46.9 (zaidi ya sh milioni 50) kutoka kwa Mfuko wa Maendeleo wa Bill & Melinda Gates kwa ajili ya kuendeleza zao la kahawa kwa wakulima wa nchi za Afrika Mashariki ikiwamo Tanzania.

Meneja mradi huo kwa upande wa Tanzania, Adolph Kumburu, alisema zaidi ya wakulima 180,000 wadogo wadogo wa kahawa katika nchi za Afrika Mashariki ikiwamo Tanzania, hasa Mkoa wa Arusha watanufaika na msaada huo.

“Ongezeko na mahitaji ya kahawa duniani litawawezesha wakulima wadogo wadogo kujipatia kipato kikubwa mara tu watakapoboresha ubora wa kilimo cha zao hilo.

“Maelfu ya wakulima ambao kwa zaidi ya miaka mitano tumekuwa tukijishugulisha nao kwa njia mbalimbali wameweza kwa kiasi kikubwa kujipatia kipato kikubwa.

“Kuongezeka kwa kipato cha wakulima hao kumekuwa na maendeleo katika familia zao, mambo ambayo yamewawezesha pia kuanza kuwasomesha watoto wao katika shule zinazotoa elimu bora,” alisema Adolph.

Msaada huo wa maendeleo wa mfuko Bill & Melinda Gates ulitangazwa hivi karibuni na Mwenyekiti mshiriki wake, mfanyabiashara Bill Gates katika kongamo la maendeleo ya uchumi duniani linalofanyika nchini Uswisi ikiwa ni hatua yake ya kwanza katika kuisaidia sekta ya maendeleo ya kilimo.

Katika hatua hiyo, mfuko huo uliozinduliwa katikati ya mwaka 2006 unatarajia kutoa dola milioni 360 katika maendeleo ya kilimo.


h.sep

juu sp.b
Habari Mpya  |  Kitaifa  |  Dar  |  Mikoani  |  Tahariri  |  Makala  |  Michezo  |  Matangazo  |  Webmaster
Copyright 2008 © FreeMedia Ltd.
Free media limited
mtaa wa Mkwepu na Makunganya, jengo la Bilicanas, gorofa ya kwanza, SLP 15261, Dar es salaam, Tanzania
simu +255-22-2126233  •  faksi +255-22-2126234  •  Selula  0713 296570