logo spc.r_ad0
sp.b_ad0
blu.strip
spc.bt_blu.strip
HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
sp.b_menu
ban
sp.b_ban
jumatatu, 28 Januari 2008
Pekua Tovuti
sp.t_sech.box sp.tafuta_w_tuma sp.t_tuma sp.r_tuma
sp.b_box sp.b_tuma
sp.b_F1
h.sep1
sp.r_men
sp.t
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari
sp.b_tuma
sp.l_men
h.sep1
sp.l sp.t sp.r
LOGIN
sp.men.l sp.men.t sp.men.r
Username
sp.b_user
sp.t-word
Password
sp.b_word
sp.t_btn
sp.b_btn
sp.b
h.sep1
tp.spc


Ghana, Morocco kufa kupona leo


na Mwandishi Wetu, ACCRA, Ghana


WENYEJI Ghana, wamepania kushinda mechi ya leo ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Morocco ili kujiwekea rekodi ya kushinda kwa asilimia 100 mechi zake tatu za hatua ya makundi.

Black Stars inahitaji sare katika mechi hiyo ya mwisho katika kundi lake A, itakayopigwa mjini hapa ili kumaliza hatua ya makundi ikiwa kinara kukwepa uwezekano wa kukutana na Ivory Coast robo fainali.

Morocco, iliyoanza kwa kuichapa Namibia 5-1 kabla ya kulala 3-2 kwa Guinea, italazimika kuishinda Ghana kama inataka kusonga hatua ya robo fainali.

Guinea na Morocco zote zina pointi tatu, lakini Guinea inaonekana kuwa na mechi rahisi dhidi ya Namibia itakayopigwa Sekondi.

Mechi zote zitafanyika kuanzia saa 2.00 usiku, kuepuka hali ya kupanga matokeo.

Ghana italazimika kufanya mabadiliko kwenye safu yake ya kiungo kutokana na kumkosa kiungo wake mahiri, Laryea Kingston anayetumikia adhabu ya kukosa mechi moja kutokana na kuonyeshwa kadi mbili za njano.

“Morocco itakuwa ngumu kwa sababu wana timu nzuri, lakini mashujaa wataonekana uwanjani,” alisema kocha wa Ghana Claude Le Roy, aliyewataka mashabiki kuwashangilia kwa nguvu.

Kurejea uwanjani kwa Sofiane Alloudi, aliyepiga mabao matatu katika mechi ya ufunguzi, kunatoa matumaini kwa Morocco kuweza kuiangusha Ghana. Nyota huyo alikuwa majeruhi.

Guinea itashuka dimbani bila nahodha wake, Pascal Feindouno anayeanza kutumikia adhabu ya kukosa mechi mbili, lakini bado Namibia itakuwa kwenye wakati mgumu.

Aidha, Namibia ambayo tayari imetupwa nje baada ya kupoteza mechi mbili, imepania kuaga Ghana kwa ushindi.

Katika mechi za juzi, baada ya kutandikwa 4-2 na Misri, Cameroon juzi ilifanikiwa kuilaza Zambia mabao 5-1, hivyo kufikisha pointi tatu.

Mabao ya Cameroon yalifungwa na Geremi Njitap katika dakika ya 28 kabla ya Job kupiga la pili dakika ya 32.

Bao la tatu lilifungwa na Emana dakika ya 44 huku la nne likifungwa na Samuel Eto’o dakika ya 66 kwa mkwaju wa penati.

Katika dakika ya 82, Job alirejea kwa mara nyingine na kupiga bao la tano huku Zambia ikipata bao la kufutia machozi dakika ya 90 likifungwa kishujaa na Felix Katongo.

Katika mchezo mwingine, mabingwa watetezi Misri, waliendeleza wimbi la ushindi kwa kuichapa Sudan mabao 3-0.


h.sep

juu sp.b
Habari Mpya  |  Kitaifa  |  Dar  |  Mikoani  |  Tahariri  |  Makala  |  Michezo  |  Matangazo  |  Webmaster
Copyright 2008 © FreeMedia Ltd.
Free media limited
mtaa wa Mkwepu na Makunganya, jengo la Bilicanas, gorofa ya kwanza, SLP 15261, Dar es salaam, Tanzania
simu +255-22-2126233  •  faksi +255-22-2126234  •  Selula  0713 296570