KATIKA hali inayoonyesha mkanganyiko wa mambo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), chama hicho tawala kimeibuka na kudai kwamba hoja ya ubadhirifu ndani ya Benki Kuu Tanzania (BoT) ilianzishwa na serikali na si Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa ...
HABARI kubwa katika gazeti hili leo inahusu kauli ya Katibu wa Uenezi na Itikadi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Chiligati, kwamba hoja ya ubadhirifu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), iliyoibuliwa bungeni na Dk. Willbrod Slaa haikuasisiwa na upinzani...
"SERIKALI yangu ina fedha nyingi, tatizo ni kuhakiki tu," ni kauli aliyoitoa Rais Jakaya Kikwete Oktoba mwaka jana alipokuwa akihutubia kwenye sherehe za Siku ya Walimu Duniani zilizofanyika mkoani Lindi ...
INAPOTOKEA sheria iliyotungwa na Bunge la Afrika Mashariki ikagongana na sheria ya nchi, sheria ya Afrika Mashariki inapewa nguvu ya kutumika na nchi husika kutakiwa kuhuisha sheria yake, ili kuondoa mgongano huo, Bunge lilielezwa jana...
MWAKILISHI wa Mkanyageni Pemba, Haji Faki Shaali (CUF), aliyesimamishwa kuhudhuria vikao vya Baraza la Wawakilishi kwa siku 21 amedai kuwa taratibu zilizotumika hazikuzingatia kanuni za mfumo wa vyama vingi ...
ZAIDI ya wagonjwa 100 waliolazwa kwenye wodi ya wazazi na watoto katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga - Bombo, wamepokea msaada wa majisafi, biskuti, sabuni na maji ya dawa (Drip), ambavyo vilitolewa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Tanga ...
MECHI mbili za mwisho za kuwania tiketi ya robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika zinapigwa leo kwa Tunisia kupepetana na Angola huku Afrika Kusini ikicheza na Senegal mjini hapa...