KWA mara ya kwanza tangu kujiuzulu kwa lazima, aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, Rais Kikwete ameelezea hisia zake kuhusu tukio hilo, ambalo anakiri kwamba lilikuja wakati usiotarajiwa. Rais alimuelezea Lowassa kuwa kiongozi aliyelitumikia taifa hili kwa ujasiri na uzalendo mkubwa...
KWA miaka miwili sasa vyombo vya habari vimekuwa mstari wa mbele kuandika kuhusu tuhuma za baadhi ya viongozi wa serikali kuipendelea Kampuni ya kuzalisha umeme ya Richmond. Tuliandika wazi wazi kuwamba kampuni hiyo imejaa ubabaishaji na kwamba inabebwa na vigogo wa serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Wakati tukiandika haya, viongozi wengi walitupuuza na kutuona wenye wivu...
HIVI karibuni, Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), lilitangaza matokeo ya mtihani wa Kidato cha Nne uliofanyika Oktoba mwaka jana. Matokeo hayo yanaonyesha kupanda kwa kiwango cha kufaulu kwa asilimia 3.65, huku shule za sekondari za serikali zikizidi kufanya vibaya ikilinganishwa na shule za binafsi...
MAANDAMANO yaliyopangwa kufanyika leo kupinga ziara ya Rais wa Marekani, George W Bush, huenda yasifanyike kutokana na maandalizi yake kusuasua, kwa kile kinachoonekana ni hofu za kiusalama...
NDEGE ndogo ya watalii, iliyoanguka na kuua watu wawili mjini hapa, ilikuwa na hitilafu kwenye injini yake. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Ng’hoboko, alisema jana kuwa ajali hiyo iliyohusisha ndege aina ya Cissna namba 5H-FUN inayomilikiwa na Kampuni ya Serengeti Ballon Safari ya Arusha, ilikuwa na matatizo ya injini...
MFUKO wa Amina Chifupa - Amina Chifupa Foundation - unatarajiwa kuandaa matamasha mbalimbali ya michezo na burudani kwa ajili ya kuchangia mfuko huo...
KITENDO cha Simba kutoka sare na Manyema FC katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyopigwa juzi, kimewatia hofu viongozi wa klabu hiyo, hata kulitaka benchi la ufundi, kufanya kazi ya ziada kuhakikisha timu inashinda katika mechi ya Jumapili dhidi ya AWASA ya Ethiopia...