BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jana lilihitimisha mkutano wake wa 10 mjini Dodoma kwa kupitisha mapendekezo yote yaliyotolewa na Kamati Teule ya Bunge ya Kuchunguza Mkataba wa Kuzalisha Umeme wa Dharura kati ya Kampuni ya Richmond na TANESCO...
SERIKALI imeipa notisi kampuni ya kushughulikia makontena katika Bandari ya Dar es Salaam, ikiitaka wakae pamoja na kujadili mkataba baina yake na kampuni hiyo...
RAIS wa Marekani, George Bush na mkewe Laura Bush pamoja na ujumbe wake, leo wanatarajiwa kuwasili kwa ziara ya siku nne nchini. Hii ni mara ya kwanza kwa rais huyo kuwasili nchini. Ziara ya kiongozi huyo ni heshima kubwa kwa nchi yetu...
MAISHA ya Watanzania yanaweza kufananishwa na usiku wa giza totoro uliomkumba msafiri ghafla akiwa njiani. Huenda akawa ameianza safari yake asubuhi iliyoonekana kuwa njema kabisa, tena akiwa na matumaini makubwa ya kufika mapema aendako, kule ambako hakutakuwa na giza tena bali nuru tele ...
CHAMA cha Wafanyakazi wa Shughuli za Meli na Bandari Tanzania (DOWUTA), kimelaani kitendo cha Kampuni ya Tanzania International Container Terminal Services (TICTS) kuongezewa muda wa mkataba kabla wa awali haujamalizika...
DAWA za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi (ARV) zinazotolewa na Bohari ya Dawa nchini (MSD), zinadaiwa kwisha muda wake wa matumizi, hivyo kuwa hatari kwa matumizi ya binadamu...
MSAFARA wa magari 15 ya abiria pamoja na pikipiki 10 za mashabiki wa bendi ya muziki wa dansi ya Twanga Pepeta International, unatarajiwa kuilaki bendi hiyo itakapowasili kesho kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K Nyerere jijini Dar es Salaam...
SENTAAFU wa kutumainiwa wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba ya jijini Dar es Salaam, Victor Costa Nampoka Nyumba, kwa sasa yu fiti na anatarajiwa kuwamo katika mechi ya kwanza ya hatua za awali za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AWASSA ya Ethiopia, itakayochezwa kesho katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ...