HABARI MPYA LA JANA MATANGAZO BEI ZETU WASILIANA NASI TUMA HABARI
ijumaa, 7 mei 2010
Yaliyopita
Pekua Tovuti

JKT yatangaza nafasi za kazi


na Andrew Chale

 

JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limetangaza nafasi za kazi kwa vijana wa kujitolea kujiunga kwa mkataba wa miaka miwili.

Taarifa kutoka Ofisi ya Habari Makao Makuu ya jeshi hilo, zinaeleza kuwa jeshi ilo litaandikisha vijana wa kujitolea kwa hiari kutoka vijijini na mijini kwa mkataba wa miaka miwili kulitumikia taifa.

Zoezi hilo, ambalo limeanza Mei mwaka huu litakuwa ni la nchi nzima huku sifa za kujiunga ni kwa vijana wenye umri kati ya miaka 18 hadi 23, elimu ya kuanzia darasa la saba na kuendelea.

Sifa nyingine ni kutokuoa au kuolewa, kutokuwa na mtoto pamoja na kutokuwa na historia ya uhalifu wa kutumia silaha ama kushtakiwa kwa makosa ya jinai.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa vijana waliokwishapitia mafunzo ama kujiunga na majeshi ya JWTZ, JKT, Polisi, Magereza, KMKM na JKU hawaruhusiwi kutuma maombi.



juu