HABARI MPYA LA JANA MATANGAZO BEI ZETU WASILIANA NASI TUMA HABARI
ijumaa, 8 juni 2012
Yaliyopita
Pekua Tovuti

Kesi ya Fundikira kuendelea leo


na Christina Mwagala

 

KESI inayowakabili askari Rhoda Robert (JKT), Mohamed Rashid (JWTZ) na Ali Ngumbe (JKT) ya kudaiwa kumuua Swetu Fundikila, itaendelea kusikilizwa leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Mahakama hiyo iliiahirisha kesi hiyo jana ili kutoa nafasi kwa mawakili wa upande wa washitakiwa, Muluge Karoli na Godifrei Uwong’a, walioomba wateja wao kupatiwa muda wa kujipanga tena kwa ajili ya kutoa ushahidi kamili.

Washitakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo Januari 23, 2010 eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Katika hatua nyingine, Meneja wa Kampuni ya MS Travel Ltd, Kessy Robert (30) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa tuhuma za kuiba sh milioni 5.3 mali ya kampuni hiyo.

Mwendesha Mashitaka, Annuciatha Leopard, mbele ya Hakimu Joyce Minde, alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Machi 28 mwaka huu, katika ofisi ya Pace, Mtaa wa Jamhuri.

Mshitakiwa alikana kosa na kurudishwa rumande hadi Juni 20 mwaka huu kesi yake itakapotajwa tena.



juu