HABARI MPYA LA JANA MATANGAZO BEI ZETU WASILIANA NASI TUMA HABARI
ijumaa, 8 juni 2012
Yaliyopita
Pekua Tovuti

‘Watanzania acheni kuwa ombaomba’


na Happiness Mtweve, Dodoma

 

WATANZANIA wametakiwa kuacha kuombaomba chakula badala yake watumie vema zana bora za kilimo ili wafanye kilimo chenye tija na manufaa kwa nchi.

Alizungumza hayo na wakazi wa mji wa Dodoma na viunga vyake, Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Rehema Nchimbi, wakati wa ziara ya wakuu wa mikoa, wilaya na makatibu tawala kutoka mikoa yote nchini waliotembelea kituo cha mradi wa usambazaji matrekta kupitia Shirka la Uzalishaji mali la SUMA JKT.

“Tumieni fursa hii kikamilifu mana ni ya kipekee kwenu ambayo itawawezesha kufanya kilimo chenye manufaa kwa mustakabali wa taifa na jamii yetu, lakini pia itatusaidia kuacha kuwa ombaomba wa chakula cha msaada,” alisema Dk. Nchimbi.

Akitoa maelezo kuhusu mradi wa kusambaza matrekta, Kanali Felix Samilami alisema kampuni ya Sinana Enterprises inakabiliwa na changamoto ya wakulima kushindwa kukopesheka.

“Mifumo iliyopo ya kibenki inamhitaji mteja kuweka dhamana kubwa zinazotambulika kisheria kwenye mifumo rasmi na kusababisha vikwazo kwa wakulima na kuwafanya kushindwa kununua matrekta hayo,” alisema Kanali Similami.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sinana Enterprises Calvin Maimu alisema lengo la ziara hiyo ni kupeleka ujumbe kwa wananchi kuhusu Kilimo Kwanza kwani wao ni watendaji wakuu wanaofanya kazi kwa ukaribu na wananchi.



juu