HABARI MPYA LA JANA MATANGAZO BEI ZETU WASILIANA NASI TUMA HABARI
jumatano, 4 julai 2012
Yaliyopita
Pekua Tovuti

Bil. 3 kupeleka umeme vijiji sita Tabora

JIBU LA SWALI LA MBUNGE Sikonge

na Mwandishi wetu, Dodoma

 

SERIKALI inatarajia kutumia jumla ya shilingi bilioni 3.8 kwa ajili ya kupeleka umeme katika vijiji sita (6) vya wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.

Hayo yalibainishwa mjini hapa jana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele, wakati alipokuwa akijibu swali la msingi wa mbunge wa Sikonge Juma Nkumba (CCM).

Mkumba katika swali lake alitaka kujua hatua iliyofikiwa na Serikali katika kuvipatia umeme vijiji hivyo vya Usanganya, Mole, Chabutwa, Ipole na Mpombwe ambavyo vinakidhi viwango vya kuwa na umeme.

Akiendelea kujibu swali hilo Naibu Waziri huyo alisema gharama hizo zitatumika kujenga kilomita 94 za njia ya umeme wa msongo kv, 33 na ufungaji wa transfoma 12 ambapo jumla ya wateja 300 wanatarajiwa kupatiwa umeme katika mradi huo.

Alisema umeme utakwenda katika vijiji vya Usanganya, Chabutwa na Ipole ukitokea Sikonge mjini ambapo umeme unaokwenda Mole utakuwa ukitokea kijiji cha Tutuo na umeme wa kijiji cha Mpombwe utatokea Mpombwe Centre.

Aidha alisema Serikali kupitia wakala wa nishati vjijini (REA) ipo katika hatua ya maandalizi ya awamu ya pili ya mradi kabambe wa umeme vijijini.

Alisema mradi huo utatekelezwa katika kipindi cha bajeti ya mwaka huu wa fedha 2012/2013 na unategemewa kukamilika baada ya miezi 24.



juu