HABARI MPYA LA JANA MATANGAZO BEI ZETU WASILIANA NASI TUMA HABARI
jumatano, 4 julai 2012
Yaliyopita
Pekua Tovuti

Wakenya kuichezesha Ngorongoro


na Ruhazi Ruhazi

 

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF), limeteua waamuzi kutoka Kenya kuchezesha mechi ya raundi ya pili ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa vijana wenye miaka chini ya 20 kati ya Tanzania ‘Ngorongoro Heroes’ na Nigeria.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema kuwa mwamuzi atakayechezesha mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili itakayofanyika Julai 29 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam atakuwa Moses Ojwang Osano.

Aidha, Wambura alisema kuwa waamuzi wasaidizi watakuwa Peter Keireini na Elias Kuloba Wamalwa, wakati mwamuzi wa mezani ‘fourth official’ atakuwa Thomas Onyango, wakati Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Charles Masembe kutoka Uganda.

“Mbali ya waamuzi hao kuchezesha mechi hiyo, pia CAF imemteua Alfred Rwiza wa Tanzania kuwa Kamishna wa mechi ya michuano hiyo kati ya Misri na Kenya itakayochezwa jijini Cairo, Misri kati ya Julai 27, 28 na 29 mwaka huu,” alisema Wambura.



juu