HABARI MPYA LA JANA MATANGAZO BEI ZETU WASILIANA NASI TUMA HABARI
jumanne, 7 agosti 2012
Yaliyopita
Pekua Tovuti

Azam U-20 waitamani Simba FC BancABC


na Clescencia Tryphone

 

TIMU ya vijana chini ya miaka 20 (U-20), ya Azam FC imetamani kushiriki michuano ya BancABC Super8 iliyoanza kutimua vumbi juzi katika viwanja vinne hapa nchini.

Wakizungumza kwa masikitiko kwenye Uwanja wa Chamazi, Mbagala jijini Dar es Salaam juzi, baadhi ya wachezaji wa timu hiyo, ambao waliomba majina yao kuhifadhiwa, walisema wanayatamani mashindano hayo, kwani hata Simba imeanza kukichezesha kikosi cha pili.

“Ukweli dada yetu, sisi uongozi wetu unakuwa kama unatutenga vile na kuwajali wakubwa, wakati wao juzi tu hapa wametoka kushiriki michuano ya Kagame, ni bora wangetuachia na sisi tucheze Super8 kama Simba walivyofanya,” alisema mmoja wao akiungwa mkono na wenzake.

Aidha, walienda mbali na kudai, wao hawana michuano mingi wala mechi zaidi ya michuano ya Uhai, ambayo huchezwa mara moja kwa mwaka, ndio maana wanawaonea wivu Simba.

Katika hatua nyingine, Azam FC juzi walianza vema michuano hiyo, baada ya kuichapa Super Falcon kwa mabao 2-0 mjini Zanzibar huku Mtibwa na Polisi Morogoro walishindwa kucheza kutokana na Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuwa kwenye ukarabati. Michuano hiyo inatarajiwa kuendelea Alhamisi.



juu