WANAFUNZI watatu bora waliofaulu mtihani wa elimu ya dini ya Kiislamu wametangazwa jana jijini Dar es Salaam.
Akitangaza matokeo hayo jana, mtaribu wa mitihani hiyo kwa shule za msingi, Suleiman Daud, alisema mitihani hiyo ilifanyika Julai 25 mwaka huu.
Aliwataja wanafunzi waliofanya vizuri kwa kupata alama 85 ni Hijra Khamis kutoka Pemba, Rehema Karungi (Kagera), na Mohamed Athuman (Dar es Salaam).
Alisema idadi ya ufaulu kwa mwaka huu ni ya wastani ikilinganishwa na ufaulu wa mwaka jana.
Alisema mitihani hiyo ni ya hiyari, ila inatambulika kiserikali lakini bado haijasajiliwa rasmi na kuwa mtihani wa taifa.